Friday, September 27, 2013

MRISHO NGASA KUIVAA RUVU SHOOTING KESHO

Kocha Msaidizi wa Yanga, Fredy Felix Minziro, amesema winga wao, Mrisho Ngasa atakuwa miongoni mwa wachezaji 11 wa kikosi chao kitakachoanza katika
mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting itakayochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho.

Ngasa ameshindwa kukitumikia kikosi cha mabigwa hao wa Tanzania Bara katika mechi tano zilizopita za Ligi Kuu Bara msimu huu, baada ya kupewa adhabu ya kukosa mechi sita kutokana na kujisajili timu mbili, Simba na Azam.

Minziro alisema wameridhishwa na kiwango kinachoonyeshwa na mchezaji huyo wakati wa mazoezi yanayofanyika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola.

"Licha ya kuikosa ligi kuu kwa muda mrefu, Ngasa bado ni mchezaji mzuri. Anafanya vizuri katika mazoezi. Kutokana na kiwango anachokionyesha, hatuna sababu ya kutomwanzisha katika mechi yetu ya Jumamosi (kesho),"

"Tunajua anakabiliwa na adhabu nyingine ya kulipa fedha za Simba, lakini suala hilo kwa sasa liko chini ya uongozi, tunaamini litashughulikiwa kabla ya mechi," alisema Minziro.

0 comments:

Post a Comment