Friday, September 27, 2013

FAST JET WAKWAMA TENA WARUDISHA NAULI ZA WATEJA

Kampuni ya ndege ya Fastjet inayoaminikia kuwa na huduma ya bei nafuu Tanzania imekwama kufikia malengo ya kusafirisha abiria kutoka Tanzania kuelekea Afrika Kusini leo.


Kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Kampuni hiyo ya Fastjet awali walidai kuwa wangeaanza Kusafirisha abiria kutoka Tanzania na kuelekaea Afrika Kusini siku ya leo lakini kabla hata ya kuanza kwa safari hiyo jana abiria ambao walishakuwa wamelipia safari hiyo walipigiwa simu na kampuni hiyo ili wakachukue pesa zao baada ya kushindwa kufanya safari hiyo.

Mpaka sasa hakuna abiria au taarifa zozote zilizotolewa na Kampuni hiyo na kueleza sababu kuu za kuahirisha safari hizo kwa muda usiojulikana.

Katika historia hii ni mara ya pili kwa kampuni ya FastJet kushindwa kuanza safari za Afrika Kusini mara ya kwanza kampuni hiyo ilishindwa kuanza safari za kwenda nchini humo baada ya kushindwa kutoa malipo ya awali kwa ajili ya kukodi ndege aina ya Boeing 737 - 300 iliyopanga kuitumia kwa safari za Cape Town - Johannesbur.

0 comments:

Post a Comment