Nilibainika
kuwa naugua ugonjwa wa Ukimwi mwaka 1988 wakati huo nikiwa na umri wa
miaka 34. Lakini, nimeweza kuishi salama hadi sasa kutokana na
kuzingatia masharti,” hii ni kauli ya Pelagia Katunzi anayeishi na
virusi vya Ukimwi (VVU).
Katunzi
ambaye sasa ana umri wa miaka 58, anasema mume wake alikufa mwishoni
mwa mwaka 1988, baada ya kupimwa na kugundulika kuwa ana ugonjwa huo.
Hii
ni kutokana na ukweli kuwa, wakati huo hazikuwepo dawa za kufubaza
virusi vya Ukimwi na kuchangia kasi ya kifo chake.
baada
ya kufahamu hali yake aliishi kwa kuzingatia masharti ya kitaalamu
ikiwamo kula chakula sahihi, kutofanya ngono holela hasa ngono zembe,
kudhibiti hofu na kutokunywa pombe.
Pia
anasema alikuwa muwazi kwa kila mwanaume aliyemtaka kimapenzi
alimfahamisha ukweli na hivyo kupunguza msongamano wa wanaume
waliokuwa wakimfuata na kumtaka awe na mahusiano nao ya kimapenzi.
“Watu
wengi wanakufa haraka kwa sababu ya kuwa na hofu, unapojitambua
ukaweza kudhibiti hofu unaishi muda mrefu bila kuugua.Lakini, ukiwa
na hofu kila wakati, unaugua kila mara na kufa haraka,” anasema.
Mama
huyo ambaye wakati mume wake anafariki alimwachia watoto wanne ambao
amewalea mwenyewe.
Anasema
katika kipindi hicho, alikuwa mdogo, mzuri, anavutia hivyo kama
asingekuwa muwazi angeambukiza watu wengi, lakini pia naye angekufa
haraka na kuacha watoto wake wakiwa wadogo.
Katika
kipindi kirefu anasema kuwa hakutumia dawa bali alizingatia masharti
hayo ya kitaalam na kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi
(ARVs) mwaka 2009.
0 comments:
Post a Comment