Wednesday, July 17, 2013

ZITTO KABWE AMTAKA JAMES MBATIA NA CHAMA CHAKE KUFIKIRI JUU YA MAAMUZI YAO.

Mbunge wa Kigoma Kasikazini Mh Zitto Kabwe amekitaka Chama Cha NCCR-Mageuzi kilichochini ya Mwenyekiti wake James mbatia na Viongozi wengine wa Chama hicho kutizama vizuri maamuzi yao ya kuipa nafasi CCM kuongoza Halmashauri ya Uvinza. 
Uongozi wa Juu wa CHAMA Cha NCCR-M umepinga makubaliano ya kuongoza kwa pamoja Halmashauri ya Wilaya Uvinza Kati ya CHADEMA na chama hicho.
Zitto amekifananisha Kitendo hicho ni sawa ya kuwasaliti wananchi wa wilaya ya Uvinza.

Tulikubaliana CHADEMA irejeshe fomu za uenyekiti, NCCR-M umakamu. CHADEMA imerejesha, NCCR-M imerejesha ya uenyekiti pia. Hivyo nafasi ya makamu Mwenyekiti imebaki na mgombea wa CCM tu"
  
Nawataka tena viongozi wa NCCR -M kutazama upya maamuzi yao. Kuipa CCM nafasi ya kuongoza Halmashauri ya Uvinza Ni kuwasaliti wananchi wa Wilaya hiyo. Madiwani wengi wa upinzani, ndio Wenye legal and political legitimacy to govern. Think Mbatia, think brother”

0 comments:

Post a Comment