Mwanafunzi
wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Tegeta jijini Dar es
Salaam, Bertha Amir (14), pichani, amejinyonga hadi kufa akipinga...........!
kulazimishwa na mama yake mzazi kusoma.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema mwanafunzi
huyo alijinyonga juzi saa 11:00 jioni, maeneo ya Tegeta Namanga,
jijini Dar es Salaam.
Alisema
marehemu alikutwa amejinyonga chumbani kwa kutumia mtandio
ulioning’inizwa juu ya dari.
Kamanda
Wambura alisema sababu za mwanafunzi huyo kujinyonga bado
hazijafahamika, lakini akasema inasadikika kuwa wakati wa enzi za
uhai wake, siku moja kabla ya kifo chake, alikuwa ameongea na mama
yake, Angelina Maiko Mshami (30), ambaye alimtaka achukue fedha kwa
ajili ya kujiandaa kwenda shule.
Alisema
mtoto huyo alimjibu mama yake kuwa hahitaji kusoma, bali anataka
kufanya kazi.
Kamanda
alisema kuwa mwili wa mwanafunzi huyo umehifadhiwa katika Hospitali
ya Mwananyamala kwa uchunguzi na kwamba, polisi wanaendelea na
upelelezi kuhusiana na kifo chake.
Akizungumza nyumbani kwake Tegeta jana jioni, mama wa mtoto huyo, Angelina
Mshami, alisema alishangazwa na kitendo cha mtoto wake kuamua kukataa
shule ghafla wakati alikuwa ana uwezo mzuri darasani.
Alisema
kuwa mtoto wake alikuwa na akili darasani akishika nafasi ya kwanza
ama ya pili wakati akisoma shule ya msingi na hivyo kumfanya afaulu
kujiunga kidato cha kwanza.
Hata
hivyo, alisema kabla ya kifo chake, binti yake alimweleza kuwa hataki
shule bali anataka kufanya kazi.
Alisema
alipomuuliza kazi gani anataka kuifanya, hakuitaja bali alisisitiza
kuwa anaifahamu mwenyewe.
Betha
ambaye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wawili katika familia yao,
alizaliwa mwaka 1999, Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.
Alianza
darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Malindi mkoani Tanga na
kufanikiwa kujiunga na Shule ya Sekondari Mtumbi na baadaye
kuhamishiwa katika Shule ya Sekondari Tegeta.
Aidha,
baadhi ya majirani waliokuwapo msibani hapo, walielezea masikitiko
yao na huzuni kuhusiana na kifo cha msichana huyo.
Marehemu
anatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea mkoani Tanga kwa mazishi
yatakayofanyika kesho kijijini Malindi.
CHANZO:
NIPASHE







0 comments:
Post a Comment