Tuesday, July 16, 2013

NINGETOKA NA MTOTO WA RAIS INGEKUWA RAHA SANAA-VANESSA


Msanii wa Kike kutoka Bongo ambae anavipaji mbalimbali kama utangazaji,Uimbaji anaefahamika kwa jina la Vanessa Mdee amefunguka na kusema kuwa kama angepata nafasi ya.........
kudate na Mtoto wa Raisi ingekuwa Rahaa.

Vanessa alifunguka hayo katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na East Africa Televison,alidai kuwa watu wanamzushia mambo mengi mpaka kusema kuwa anatoka na mtoto wa Presidar hivyo yeye akasema kama ingekuwa hivyo kwake ingekuwa raha sanaaaa.

Vanessa alisema kuwa alikuwa hajiamini kufanya muziki ingawa muziki ndiyo kitu alichokuwa akikipenda zaidi, hapo ndipo likaibuka swali umewezaje kufanya muziki ikiwa hujiamini kufanya muziki.

katika kujibu swali hili ndipo alipofunguka kuwa kama angepata nafasi ya kutoka au kuwa na mahusiano na mtoto wa Raisi kwake ingekuwa rahaa sanaa.

Kipaji cha muziki cha Vanessa Mdee kilianza kujulikana baada ya kusikika kwenye wimbo wa AY ‘Money’ na baadae kuidhihirisha jamiii kwenye ‘Me and You’ alioshirikishwa na Ommy Dimpoz

Mwanzoni mwa mwaka huu Vanessa alitoa single yake ya kwanza, ‘Closer’ ambao umemtambulisha vizuri kwa Watanzania walio wengi.



0 comments:

Post a Comment