12:03 AM

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Uzoefu wako hauwezi kukusaidia kufikia maamuzi katika mambo ya maendeleo, ni lazima kuwashirikisha wengine
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)...............!
Taarifa unazoendelea kuzihodhi zitakuletea matatizo, huu ni wakati wa
wewe kuwa muwazi katika mambo yako kama unataka kufanikiwa.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Washirika wako na watu wako wa karibu watakutisha kutokana na taarifa
watakazokupa kukuhusu wewe, lakini hayo yasikusumbue akili endelea na
mipango yako
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Jaribu kuwa
karibu na ndugu zako au watu wanaokuzidi umri hali hiyo itakuongezea
nafasi ya kuwa na mafanikio katika maisha yako.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Kuna watu wanatengeneza mazingira mabaya ya kukuharibia mambo yako, shikilia msimamo wako na usikubali kuyumbishwa utakwama.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo kila mmoja ataonekana kupendezwa na wewe, hali hii inaweza
kukufanya kuanguka kwenye caguo baya, unatakiwa kuwa makini.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo Kuna mambo hautaweza kuyafanya peke yako ni lazima kuomba msaada kwa wengine, bila hivyo utaendelea kukwama.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Hisia zako zinaonekanakuwa na nguvu kuzima hali ya khofu, lakini uwezo unakosekana kwa sbabu ya kutokujiamini.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo ni bora ukadharau mipango yote iliyokunyima nafasi awali, mpenzi au rafiki wa karibu anaweza kuwa msaada kwako.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Maamuzi unayolenga kuyatoa yanaonekana kuegemea upande mmoja, wengine wanaweza kujenga chuki kwako wape nafasi.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Leo inawezekana ukashindwa kumuelewa mwenzako kwa sababu ya kuwa naye mbali, huu ni wakati muafaka wa kuwa naye karibu
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Yaliyokutokea jana hayawezi kufanana na yale ambayo yatakutokea leo,
kwa hivyo kama ulikwama au kama hukufanikiwa, jana leo jaribu tena mambo
yanaweza kuwa mazuri.
0 comments:
Post a Comment