Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa
2013/2014 inaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu kwa timu zote 14
kuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
Hata hivyo, kabla ya
ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii-
Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam
itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi za VPL za Agosti
14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu,
Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Nyingine ni Mgambo
Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na
Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera
Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na
Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).
Mzunguko wa kwanza wa
ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika
Aprili 27 mwakani







0 comments:
Post a Comment