Kiungo
mwenye kiwango cha juu katika Soka la Bongo achezaye timu ya soka ya
Simba ya jijini Dar es Salaam na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa
Stars), Amri Kiemba, amesema kwamba
hafikirii kurejea Yanga wala
timu nyingine yoyote nchini kwani malengo yake sasa ni kucheza soka
la kulipwa barani Ulaya na kwingineko nje ya Tanzania.
Uongozi
wa Simba kupitia mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage, umetangaza kuwa
wamepokea 'ofa' kutoka klabu moja ya Uturuki ikimuhitaji kiungo huyo
kwa dau ya dola za Marekani 240,000 (Sh. milioni 379) na kupewa
mshahara wa dola za Marekani 15,000 (Sh. milioni 24) kwa mwezi.
"
Kwa sasa nawaza kucheza nje ya nchi na sitakataa ofa nitakayoipata,"
alisema Kiemba.







0 comments:
Post a Comment