Tuesday, July 23, 2013

NANI KUIBUKA KIDEDEA KATI YA SIMBA NA YANGA OKTOBA 20 ?

Watani wa jadi Simba na Yanga wanatarajiwa kushikana mashati tena Usiku wa 20 Oktoba katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watapokutana kwa mara ya kwanza katika mechi ya watani wa jadi msimu huu .


Kwa Mujibu wa Ratiba mpya iliyotolewa jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaonesha watani hao watakutana tarehe 20 Oktoba.

Ikumbukwe kuwa kwa mara ya mwisho watani hao wa jadi walipokutana katika ile mechi ya kufunga msimu mwezi wa tano tarehe 26,Yanga ilimgalagaza 2-0 Simba,na kuchukuwa ubingwa huku Simba Sports Club ikikamata nafasi ya Tatu baada ya Azam Fc waliochukuwa nafasi ya pili katika Ligi ya Vodacom.

0 comments:

Post a Comment