1:12 AM

KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo
kuna dalili ya kushindwa kupata kila unachokusudia wakati, huu ni
vyema ukajipanga upya ili uweze kukabiliana na hali iliyo mbele
yako.
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Kuwa makini na idadi
kubwa ya marafiki wanaokuzunguka, kuna uwezekano wa kushindwa
kutimiza malengo yako kutokana na misaada unayotoa.
MASHUKE -
VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Tafuta njia ya kukabiliana na hali
inayokukabilikwa sasa bila ya msaada kutoka kwa wengine, mambo
yataendelea kukuelemea kwa muda mrefu.
MIZANI - LIBRA (SEPT
24- OCT 23)
Uwezo wako kifedha utaongezeka kama ambavyo kwa muda
mrfu umekuwa ukifikiria, vile vile utakuwa na wakati mzuri kazini
hasa wiki hii.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Jitihada
zako hazitakuwa na manufaa kama utashindwa kupokea ushauri, ni wakati
unaopaswa kubadilika ili uweze kusonga mbele
MSHALE -
SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Kuna mawazo tofauti utakumbana nayo
siku ya leo , usisite kupokea ushauri na vile vile usichanganye
shughuli zako zinazokuingizia kipato na mapenzi.
MBUZI -
CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Utapata wakati mzuri wa kukutana na
jamaa zako wa karibu ama ndugu zako katika familia kwa ajili ya
mazungumzo, jaribu kutafuta njia mbali mbali zitakazikuwezesha
kufikia leongo lako.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Kazi au shughuli zako zinaweza kuigia dosari kama utashindwa kuwa
muangalifu, wale unaowaamini wanaweza kukuweka kwenye wakati mgumu
hasa siku ya leo.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Ukifanya uchunguzi wa jambo linalokusumbua kwa muda mrefu utapata
jibu, na mambo yako utaona yanakwenda vyema, fanya maamuzi
mapema.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo ni siku nzuri
kuwa karibu na familia yako, kuna mambo utayagundua bila ya
kutarajia, kuwa makin i na majirani zako, wengine wanaweza kuleta
matatizo.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Usijiamini
sana katika maamuzi ambayo unapaswa kuwashirikisha na wengine,
unaweza kujikuta ukiingia kwenye matatizo na mzigo kuwa wako peke
yako.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Mwaliko
utakaopokea siku ya leo utakuwa na manufaa, tumia nafasi hiyo
kujifunza mambo mbali mbali, na mwisho wa siku kuna kitu
usichokitarajia utakipata.
0 comments:
Post a Comment