Monday, July 22, 2013

ALIYEIBA KICHANGA CHA MWEZI MMOJA HOSPITALI ADAKWA NA POLISI,AMESEMA ALISHIRIKIANA NA DAKTARI KUIBA KICHANGA HICHO.

Mama aliyefahamika kwa jina la Aniseth Swai mwenye Umri wa miaka (48), amedakwa na Polisi Wilaya Mkuranga, mkoani Pwani, kwa tuhuma za kuiba kichanga cha mwezi mmoja chenye jinsia ya kike.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Juma Yusuph, alisema mwanamke huyo alikamatwa juzi, saa 3.00 usiku, wilayani humo.

Alisema alipohojiwa, mwanamke huyo alikiri kuwa mtoto huyo si wake na kwamba, alimpata katika Hospitali ya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Kamanda Yusuph alisema mwanamke huyo alidai kuwa yeye hana mtoto na alikubaliana na daktari hospitalini hapo kuwa iwapo mtu atajifungua, atamwibia mtoto na kumpa amlee.

Alisema hata hivyo, hakumtaja daktari huyo kwa madai kwamba, hajui jina lake na anapoishi.

0 comments:

Post a Comment