Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
ameagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja
na makampuni ya simu za mikononi nchini kukutana mara moja.......
kutafuta
jinsi gani ya kumaliza mvutano wa kodi mpya ya kadi za simu hizo za
mikononi.
Rais
kikwete ametoa maelekezo hayo jioni ya jana, Jumanne, Julai 23, 2013
wakati alipokutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa makampuni ya
simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel katika kikao cha pamoja
kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais
Kikwete amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya
Wizara hizo za Serikali na makampuni ya simu yawe ya kupendekeza
jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni 178 ambazo zitapotea katika
Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za simu za mikononi
italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa
Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.
Rais
Kikwete amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena
kuifuta moja kwa moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata
fedha za kujaza pengo hilo la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge
limezipangia matumizi.
“Nawaombeni
kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja
tutafute namna gani tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178
endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito
na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete
amewaambia wawakilisho hao.
Katika
Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh.
1,000/= kwa mwezi kwa kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya
mawasiliano kwa kutumia simu ya mkononi.
0 comments:
Post a Comment