2:02 AM
SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG
22)
Unaonekana kupenda kazi yako lakini hakuna anayejali
unayoyafanya, yupo usiyemtarajia atakuja na jibu zuri kwako.
MASHUKE
- VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Weka msisitizo zaidi katika yale
unayotarajia kuyapanga wakati huu, kuna faida kubwa iko mbele yako,
maisha yanaweza kubadilika
MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Masuala ya pesa yatakuingiza kwenye wakati mgumu leo hii, weka
mikakati mipya ya kuziba mapengo yatakayotokea.
NGE - SCORPIO
(OCT 24- NOV 22)
Kutofanya lolote na badala yake kuangalia mambo
yanavyokwenda leo hii ni jambo zuri sana na la maana kwa upande
wako
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Jumatano ya
leo yale Yanayosemwa yatakuingiza matatizoni kama utaendelea
kuyasikiliza, si kila jambo linaweza kuwa na maana kwako.
MBUZI
- CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Mahusiano yako yatajengwa namna
unavyotaka, usikubali ushawishi usioweza kuutekeleza, vinginevyo ni
bora kuacha.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Yanayoendelea kutokea kwa sasa yasikunyime nafasi ya kufanya
maamuzi, kila jambo litakwenda kama unavyotarajia.
SAMAKI –
PISCES (FEB 20- MACH 20)
Usikubali kupokea ushauri kutoka kwa
wengine, ndio nafasi yako ya kusonga mbele, usidharau hata wale
usiowategemea.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Utahitaji
busara badala ya nguvu ili kumaliza tofauti na mwenzako, usipokuwa
makini utakaribisha matatizo zaidi,
NG’OMBE – TAURUS
(APR21 – MAY 20)
Hutapata shida kama utaanzisha mahusiano aidha
ya kikazi au ya kimapenzi kwa siku ya leo, kama hujiamini ni bora
kuendeleza na msimamo wako.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Wengine wanaweza kukuangalia vibaya lakini hilo lisikupe wasiwasi
endelea na msimamo wako na kila jambo litafanikiwa.
KAA -
CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo ni jumatano nzuri sana kwako mambo
yako mengi yatatengamaa na kujikuta uikamilisha kila jamo lako pamoja
na kwamba utapata mapingamizi ya hapa na pale.
0 comments:
Post a Comment