Wednesday, July 10, 2013

PINDA AMEPOTEZA SIFA ZA KUWA WAZIRI MKUU.


   
Zikiwa zimepita siku kadhaa toka Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kukaa na kutoa Msimamo wake juu ya mambo mbalimbali ikiwemo Rasimu ya Katiba,Vurugu na fujo wafanyiwazo viongozi na wananchi na Polisi pamoja na Kauli aliyoitoa bungeni Waziri mkuu kuhusiana na Polisi na raia.

   Kamati Kuu inaamini kwamba Waziri Mkuu................
amepoteza sifa za kuendelea kuwa Waziri Mkuu na inaungana na wananchi na taasisi ambazo zimedai Waziri Mkuu awajibike au awajibishwe kutokana na kauli yake hiyo. Aidha, Kamati Kuu inawaelekeza Wabunge wote wa CHADEMA washirikiane na Wabunge wengine wote wenye mapenzi mema na nchi hii na ambao wanaamini katika utawala wa sheria waanzishe mchakato wa kumpigia kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu kupitia Bunge;

   Kamati Kuu imewataka Jeshi la Polisi kama sehemu ya jamii ya watanzania kupuuza kauli ya Waziri Mkuu katika utekelezaji wa kazi zao kwa kuwa kauli hiyo ni ya uvunjifu wa Katiba na Sheria na inachochea uvunjifu wa amani.

0 comments:

Post a Comment