Wakali wa Filamu Bongo wanaofanya poa sana katika Tasnia
hiyo namzungumzia Mzee King Majuto na Mwanae kikazi JB ambao awali walifanya
kazi na kuwabamba watu wengi kutokana na Swaga za Mzee Majuto na JB katika kazi
hiyo iliyokwenda kwa jina la ‘Nakwenda kwa
Mwanangu’, akimshirikisha gwiji,‘King Majuto’ wajipanga kuja na Shikamoo Mzee
Siku za karibuni
Mtayarishaji na muigizaji Jacob Stephen aliingiza sokoni kazi yake iliyokwenda
kwa jina la Zawadi Yangu inayoendelea
kukimbiza sokoni kwa sasa, muigizaji nyota
wa filamu nchini, Jacob Stephen 'JB' yupo mbioni kuachia kazi nyingine
iitwayo 'Shikamoo Mzee'.
JB alisema kuwa filamu
hiyo imewashikirikisha wasanii nyota kama Chuma Suleiman 'Bi Hindu', Amri
Athuman 'King Majuto' na Shamsa Ford.
"Baada ya kuwapa
mashabiki wangu 'Zawadi Yangu' safari hii wajiandae kupata burudani
nyingine kupitia 'Shikamoo Mzee' ambayo
nimeigiza tena na King Majuto, Bi Hindu na wakali wengine," alisema JB.
0 comments:
Post a Comment