Hili ni swali ninalo
jiuliza kama ambavyo watu wengi wenye mtizamo kama wangu wanavyojiuliza swali
hili, Jana usiku Mshambuliaji ambae ni tegemeo wa Mabingwa wa ligi Kuu ya soka
kutoka Burundi katika timu ya Vital'O, ametua Tanzania kufanya mazungumzo na kujiunga
na Club ya Simba Sports.
Tambwe ambaye aliibuka
mfungaji bora katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe
la Kagame) kwa kufunga magoli sita na kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa kwanza
wa michuano hiyo, atasaini mkataba wa miaka miwili katika Club ya Simba.
Sinahofu na kiwango cha
Mchezaji huyu lakini najiuliza ujio wa Tambwe Msimbazi utaleta Uzima na ufufuo
katika Club hiyo?
Simba Sports Club msimu
uliopita ilimaliza ikiwa ya tatu na kukosa tiketi ya kushiriki mashindano ya
kimataifa mwakani.
0 comments:
Post a Comment