Shirika la Viwango (TBS) limepiga marufuku uuzaji,
ununuzi na matumizi ya mafuta ya kula ya aina ya Oki, Viking na Asma baada ya
kubainika kuwa hayana ubora na hatari kwa afya za watumiaji.
Kwa mujibu wa Tangazo lilitolewa na Shirika la Viwango
nchini (TBS)
kwa baadhi ya vyombo vya habari jana, yeyote atakayekiuka agizo
hilo atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 2 ya
mwaka 2009.
Tangazo hilo lilisema TBS ilinunua mafuta hayo
yanayozalishwa nchini Malayasia na kuingizwa kupitia njia za panya, kusambazwa
sokoni na kubainika kuwa hayajakidhi matakwa ya kiwango cha kimataifa
kinachotumiwa nchini.
“Matokeo ya uchunguzi wa
sampuli zake yalibainika kuwa yameshaharibika kabla ya
kufikia ukomo wa matumizi kutokana na kutosafishwa ipasavyo, ni machafu kutokana na kuchanganyika na maji
hivyo vigezo vya ubora wa mafuta
havikufikiwa.”
Kwa msingi huo, TBS imewataka wauzaji wa mafuta hayo kuyaondoa sokoni mara moja na wateja kuacha kuyanunua hadi
hapo itakapothibitika kuwa yamefikia kiwango kinachotakiwa.
0 comments:
Post a Comment