Wednesday, July 10, 2013

NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI TAREHE 11/7/2013


KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Masuala ya pesa yatakuingiza kwenye wakati mgumu hasa kwa siku ya leo, weka mikakati mipya ya kuziba mapengo yatakayotokea.


SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Kutofanya lolote na badala yake kuangalia mambo yanavyokwenda ni jambo la maana sana kulifanya siku ya leo.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Mambo yanayosemwa yanaweza kukuingiza matatizoni kama utayasikiliza, si kila jambo linaweza kuwa na maana kwako.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Mahusiano yako yatajengwa namna unavotaka, usikubali ushawishi usioweza kuutekeleza, vinginevyo ni bora kuacha yale unayotaka kuyafanya.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Yanayoendelea kutokea kwa sasa yasikunyime nafasi ya kufanya maamuzi, kila jambo litakwenda kama unavyotarajia, leo ni siku nzuri kwa mipangilio yako ya kikazi,

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Siku ya leo usikubali kupokea ushauri kwa wengine, hii ndio nafasi yako ya kusonga mbele, usudharau hata wale usiowategegemea,

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo tumia sana busara badala ya nguvu kama unavyofikiria ili kumaliza tofauti na mwenzako, usipokuwa makini utakaribisha matatizo zaidi.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku ya leo hutopata shida kama utataka kunzisha mahusiano mapya kama hujiamini bora kuendelea na msimamo wako,

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo wengine wanaweza kukuangalia vibaya lakini hilo lisikupe wasiwasi, endelea na msimammo wako na kila jambo litafanikiwa.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Leo inaonekana watu wengi watataka kuwa karibu nawe na lakini wengine wanaweza kuwa na nia mbaya, usipoteze muda kwa kuwa karibu na watu wa aina hiyo hata kama utawabaini mapema.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Wewe unaonekana kupenda kazi yako lakini hakuna anayeonekana kujali kujali uyafanyayo, yupo ambaye humtarajii atakuja na jibu zuri kwako

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku ya leo weka msisitizo zaidi katika yale uanyotaka kuyafanya hasa kwa wakati huu, kuna faida kubwa ambayo iko mbele yako maisha yanaweza kubadilika.


0 comments:

Post a Comment