Thursday, July 11, 2013

WASANII BLACK RHINO/PROF JAY WAFIWA NA MAMA YAO

BLACK RHINO AKIWA NA MKEWE
Msanii Nichorus Haule A.K.A Black Rhino ambae ni mdogo wa Msaniii Mkongwe wa Bongo Fleva Joseph Haule alimaarufu kama Prof Jay wamepatwa na msiba jana baada ya Mama yao kufariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospital ya Tumbi alipopelekwa baada ya Kugongwa na Gari majira ya jioni jana.


Mama Rosemary Majanjala ndiye mama mzazi wa Black Rhino na PROF JAY ambaye alipata ajali ya kugongwa na gari akiwa maeneo ya nyumbani kwa mwanae Prof huku Mbezi Mwisho.



Msiba upo nyumbani kwa Prof Jay Mbezi Mwisho mbele kidogo ya stendi mpya ya mabasi .
R.I.P Mama Rosemary



0 comments:

Post a Comment