Monday, July 15, 2013

BEN PAUL&BELLE9 EPUKENI PROPAGANDA-RAMA DEE


Msanii Rama dee ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la KAMA HUWEZI Huku akiwa amempa shavu Lady Jaydee amewataka wanamuziki wenzake ambo ni Ben paul na Belle 9 kuachana na propaganda kwani wanauwezo mkubwa wa kuimba,kuandika na sauti nzuri ambazo zitawafanya wafanye kazi na kupokelewa vizuri siki zote na FANS WAO kutokana na uwezo wao.

epukeni propaganda mnaweza sana...naskiliza Ngoma zenu hapa kila baada ya neno na sauti safi sana MAJANJA!!

Rama Dee katoa kauri hiyo kutokana na ukweli kwamba soko la muziki wa TANZANIA kwa sasa limeingiliwa na aina fulani ya Siasa,unyonyaji na ukandamizwaji kwa wasanii kisaikolojia,kiuchumi,na hata katika uelewa maana kuna kundi la watu ambao kazi yao ni kuhakikisga wananufaika kupitia migongo ya wanamuziki na kuwapandikizia nidhamu ya woga katika kazi zao,jambo ambalo humpelekea msanii kufa kisaniii mwenyewe pindi akishindwa kutimiza matakwa ya kundi hilo.



0 comments:

Post a Comment