Kajala
amefunguka hayo leo...........
alipokuwa akichat na Fans wake katika KIKAANGONI
LIVE CHAT inayoendeshwa na East Africa Television kupitia ukurasa
wake wa Facebook ambapo Fans wanapewa nafasi kuuliza jambo na yeye
kulijibu.
Mbali
na kukanusha tetesi hizo kuwa anatoka na Peti Man ameeleza kuwa yeye
bado ni mke halali wa Faraja Chambo kwa kuwa walifunga ndoa hivyo
kinachoweza kuwatenganisha ni Kifo tu na si jambo jingine kwa misingi
na imani ya dini.
AELEZEA
MAHUSIANO YAKE NA WEMA.
Fans
wengi walikuwa wakitaka kujuwa mahusiano yake yeye na Wema Sepetu kwa
sasa na hili limekuja baada ya tetesi kuvuma kuwa hawana mahusiano
mazuri na Wema Sepetu ambaye ndiye aliingia mfukoni mwake na kutoa
pesa kwa lengo la kumuokowa kutofungwa Jela.
Kajala
alisema kuwa kwa sasa hawana Tofauti yoyote ile na Wema kwani kila
kitu kimewekwa sawa na tofauti zimekwisha kwa maaana hiyo ni poa sana
tu.
UPENDO
WAKE KWA P-FUNK
Kama
kawida unapokuwa mtu maarufu watu huitaji kujuwa mambo yako mmoja
kati ya wadau aliuliza swali kuwa Bado unampenda P-Funk Majani? Bila
woga mwadada Kajala akasema kuwa bado anampenda P-Funk Majani kwa
kuwa ni Baba wa Mtoto wake kipenzi Paula.
0 comments:
Post a Comment