Friday, July 12, 2013

NYOTA YAKO LEO IJUMAA TAREHE 12/7/2013


KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Kuna njia zaidi za kukusaidia kutimiza malengo yako, mambo mengi unayoyafanya kwa wakati mmoja yatakuingiza katika wakati mgumu, kwa hivyo unatakiwa kinyota uwe muangalifu sana.


SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Ukiona mambo yanakwenda tofauti na matarajio hasa siku ya leo, tambua kwamba kuna jambo unashindwa kulitimizia ahadi, kwa hiyo likamilishe jambo hilo na mambo yatafunguka.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Leo hii utakutana na watu ambao wanaweza kukuweka kwenye mashaka kutokana na kauli zao kwako, jambo hilo lisikusumbue akili yako kaa au shikilia msimamo wako na mambo yatakwenda vizuri.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Ijumaa ya leo usikubali kufanywa mjina, kuna watu wanajaribu au watajaribu sana kukuingiza au kukutumbukiza kwenye mambo au kazi ambazi hazitakuwa na faida kwako, epukana nao na kuwa makini.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo maandalizi ya shughuli zako muhimu hayatafanikiwa bila kuwa karibu na wale ambao umewaacha mbali au kuwadharau kwamba hawawezi kukusaidia, jaribu kuwapa nafasi na utaona faida yake itakavyokuwa.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Ijumaa ya leo ni muhimu sana kwako, unaweza kubaini dalili za mahusiano kwenda vibaya, taarifa utakazopata kuhusu hayo mahusiano yako zinaweza kukuvunja moyo

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Usidharau kile kinachokuja kirahisi na ukakitumia kirahisi, hii ni bahati ambayo haiwezi kutokea tena kuwa makini na tuliza akili zako kwa kila unalofanya

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Ongeza umaarufu wako katika kazi mbali mbali, kutana na watu jitambulishe, shirikiana nao tafuta ushauri, hayo yote yanaweza kukufanya uweze kufanikiwa kwa kila jambo ambalo unataka kulifanya.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Inaweza kukuchukua muda mrefu kuwatambua wabaya wako, hata hivyo usiwe na khofu kwani kuna dalili watajitokeza wenyewe na utawatambua.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Huu ni muda wa wewe kuwa na nguvu, kazi zako au mipango yako itafanikiwa na kwenda mbele na hii ni kutokana na juhudi zako na ushirikiano na watu wengine.

NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mahitaji ya kifamilia yataongezeka na kukuweka kwenye wakati mgumu, huu ni muda wa kuongeza juhudi ili uweze kujiakamilisha na kwenda na wakati.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Unaweza kujua nini kinakusumbua kwa kufanya yale yanayolekezwa kwako , unashauriwa kinyota usidharau taarifa utakazopata siku ya leo zitakusaidia kukufungulia milango ya kipato.


0 comments:

Post a Comment