MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN
21)
Siku ya leo ni mbaya kwako jambo lolote utakalofanya hata liwe
zuri vipi litakugeuka, nyota zinakushauri kuwa ahirisha mipango yako
yote hasa kwa muda wa asubuhi na ikiwezekana mpaka kesho mchana.
KAA
– CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Siku ya leo sio nzuri sana kwako,
kama ni mfanya biashara utakumbana na hasara au mikosi na biashara
unayoifanya inaweza kukwama. Kama ni mkulima utapoteza mazao yako
kama umeoa basi kunaweza kukatokea ugomvi na mkeo, kama ni mfanyakazi
kuwa muangalifu sana ofisini na kama una mpenzi leo msionane nae
mnaweza mkagombana na kuachana.
SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG
23)
Siku ya leo mambo yako mengi yatafanyika kwa haraka kuliko
ulivyotegemea. Utapata ahadi za ukweli na zenye mafanikio katika
nyanja zote ziwe za kifedha kimaisha na kimapenzi, vile vile utapata
habari nzuri kuhusu watoto au watoto wako watakufurahisha
MASHUKE
– VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Wiki hii kuna dalili ya kupata fedha
na heshima kubwa katika jambo lako ambalo unalitarajia. Kama hujaoa
utampata wa kumuoa na kama hujaolewa ndoa ipo njiani inakuja. ndoa
hiyo kwa nyote wawili mke na mume itadumu kwa muda mrefu na itakuwa
na mafanikio makubwa.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Leo
mpaka jumatano utapata habari nzuri kutoka kwa rafiki yako wa mbali
ambayo itakufanya uache kazi yako uliyo nayo sasa. Hata hivyo
mafanikio yako makubwa yatakuja baada ya wewe kufanya mabadilkiko
aidha ya kikazi au kibiashara au makazi. Kuma huna shughuli yoyote
jaribu kuanzisha biashara yoyote utapata mafanikio.
NGE -
SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo inaonekana utasononeka sana na roho
kuuma kutokana na vitendo vibaya utakavyofanyiwa na marafiki zako
ambao wanajifanya wanakupenda sana. Na kama una mpenzi wako kuwa
macho sana maana marafiki hao waandangaya ili afunge ndoa na mpinzani
wako mkubwa.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Siku ya
leo jihadhari sana kudanganywa, usimwamini mtu yoyote katika jambo
lolote na kama unataka kulifanya hilo jambo jaribu sana kufanya
uchunguzi kabla ya kulifanya. Nyota zinaonyesha kwamba kuna dalili ya
kupoteza fedha au mali, Tafdhali jihadhari msana.
MBUZI -
CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Kama ulikuwa umedhamiria kufanya
safari ya karibu au mbali huu ndio wakati wako. Kama una kesi basi
fahamu kwamba kesi hiyo utashinda, na kama ulikuwa na jambo lolote
ambalo lilikuwa limekwama litafunguka. Unachotakiwa kufanya ili
kufqanikiwa ni kuwa makini katika ufuatiliaji tu.
NDOO
–AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku ya leo jaribu kuwa
muangalifu katika kujitetea kwa makosa uliyoyafanya na unapozungumza
na mtu yoyote hata awe mdogo au mkubwa chunga sana matamshi yako.
Kama una mawazo yako bnafsi usiwalazimishe watu wakubaliane nayo.
Katika mazungumzo yoyote leo jaribu kuwa mpole na uwaonyeshe watu
kwamba unaweza ukataubu . ukifanya hivyo utafuzu jambo lako.
SAMAKI
– PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo jaribu sana kuwa na
tahadhari, hiyo haraka yako ya kufanya mambo itakuletea hatari na
matatizo sana mbele yako.Unaweza hata kupigwa na kuumizwa usipokuwa
makini na mambo yako.
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Siku
ya leo kuna maneno au ugomvi wa maneneo utakaotokea kati yako na
rafiki yako au na watu wa familia yako. Mzozo huo utakuathiri sana
kikazi na kibiashara. Vinginevyo tegemea kupata habari ya kupona kwa
afiki yako ambaye alikuwa anaugua.
NG’OMBE – TAURUS (APR21
– MAY 20)
Siku ya leo yale yote uliyokuwa unayataka au
uliyoyadhamiria yatakuwa. Na utakutana na marafiki wakweli na
waaminifu watakaokuongoza katika njia nzuri za mafanikio ya kimaisha.
Tegemea kupata habari nzuri kuytoka nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment