Monday, June 3, 2013
LADY JAYDEE KUFANYA SHOW 14 JUNE
Msanii Lady Jaydee A.K.A “Anaconda” ametangaza rasmi tarehe yake ya kufanya show ya Miaka13 toka ameanza kufanya muziki siku ya Ijumaa ya Tarehe 14 mwezi june baada ya kuairisha show yake kufuatia kifo cha Msanii Albert Mangwear kilichotokea siku ya tarehe 28 nchini South Afrika.
Lady Jaydee amesema sababu ya kuchagua siku hiyo ni kwamba siku ya Tarehe 13 Atakwenda Mahakamani kusikiliza Kesi inayomkabili
aliyofunguliwa na wamiliki wa Radio ya watu,na siku inayofuta itakuwa show ya Miaka kumi na 13 na tarehe 15 atasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Lady Jay Dee ametumia akaunti yake ya twitter kuiweka wazi tarehe ya show yake alipokua akijibu swali la fan wake ambae atasherehekea siku moja ya kuzaliwa na msanii huyo (June 15).
0 comments:
Post a Comment