Monday, June 3, 2013
WAKALI WA BONGO FLEVA KUJULIKANA JUMAMOSI HII
Mashindano ya kuwapata wasanii bora waliofanya vizuri katika mwaka uliopita yatafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 9 katika ukumbi wa Mlimani City na kurushwa Live kupita Kituo cha Televison cha ITV .
Kwa mujibu wa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe amesema kuwa kwa mwaka huu wamejiandaa kuweka luninga kubwa ili watu wapate fursa ya kutizama zoezi hilo huko waliko na kwa kuanza kutakuwa na skrini kubwa Mabatini (Mwanza),CCM mkoa( Moshi) pamoja na Uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Shughuli za utoaji wa Tuzo hizo zinatarajiwa kuanza mida ya saa Tatu Usiku na kupambwa na Burudani Mbali mbali kutoka kwa wasanii wetu.
0 comments:
Post a Comment