Friday, May 24, 2013

YANGA NI NYUMBANI KWANGU-NIYONZIMA



Kiungo mchezeshaji kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima amesema kuwa yanga ndio nyumbani kwake na si timu nyingine kwani aichezeapo Yanga huwa anakuwa na furaha na kuwa malengo yake ni kuisaidia timu hiyo kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano mbalimbali.

Niyonzima amesema hayo leo alipokuwa akisaini mkataba wa miaka miwili na Club hiyo ya Yanga

Nawashukuru wanachama, washabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga kwa kuwa naye muda wote, Yanga ni nyumbani kwangu kwani najisikia furaha kuichezea timu hii na malengo yangu ni kuisadia ili iweze kufanya vizuri katika upatashindano ya kimataifa”

Akiongea na waandishi wa habari makao ya klabu ya Yanga, katibu mkuu Lawrence Mwalusako amesema wameamua kumuongezea mkataba mchezaji huyo kufuatia kuuhitaji mchango wake kwani katika kipindi chake cha miaka miwili ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kutoa mchango mkubwa.

kumekua yakiongelewa mengi juu ya mchezaji wetu Niyonzima, baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikitoa taarifa za kupotosha juu yake ukweli leo umedhihirika kwamba Niyonzima ni mchezaji wa Yanga na ataendelea kuitumikia kwa miaka miwili”

Haruna Niyonzima alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza Julai 2011 akitokea katika timu ya APR nchini Rwanda ambapo katika miaka yake miwili aliyoichezea timu ya Yanga amefanikiwa kuisadia kupata makombe mawili ya ubingwa wa Ligi Kuu 2012-2013 na Kombe la Kagame 2011-2012.

0 comments:

Post a Comment