![]() |
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako |
Dar
es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne
mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza
la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango
vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari
ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha
kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57,
huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo
pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo
cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa,
ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka
asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia
asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao
awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda
na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa
matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri
kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37
ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji
wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado
unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na
matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule
mapema,” alisema Nchimbi.
Pia
alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo
ya awali
Matokeo
ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk
Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756
waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu
kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia
6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia
28.1.
Katika
matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata
sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo
yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni
asilimia 43.
Hata
hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha
kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa
matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu
ikilinganishwa na awali.
Maofisa
mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita
kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la
matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada
ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo
hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida
isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo
umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Source
Mwanachi.
0 comments:
Post a Comment