Sunday, May 12, 2013

NYOTA ZENU LEO JUMATATU: 13/5/2013


NG’OMBE – TAURUS (APR 21 – MAY 20)
Siku ya leo ukimuona mtu anapaka rangi, hiyo ni dalili kwamba ile habari ambayo ulikuwa unaifuatilia utaikosa au utafichwa bila ya sababu ya msingi. Unashauriwa kutokata tama upesi kwa kila kitu. 

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Siku ya leo ukimuona Kasuku anaimba kwa sauti ndogo, basi hiyo ni ishara kwamba yule mtu uliekuwa unamtegemea atakudanganya na kukuibia bila ya kutegemea kutokea kwa hali hiyo. Usimuamini kila mtu kwa Siku ya leo.

KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Leo ukimuona Njiwa Mweusi, basi ujue utapata mikosi na mabalaa kila utakapokwenda, iwe kwa shughuli za kikazi au mapanzi. Heshima itapetea na utafedheheshwa bila ya kutarajia.

SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG 23)
Siku ya leo ukikutana na Daktari unayemfahamu, hiyo ni dalili kwamba utapona au mgonjwa wako atapona maradhi yake yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mlefu. Jaribu kuwa mwangalifu na matembezi ya kila siku jioni.

MASHUKE – VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Siku ya leo ukikutana na mtu yoyote unayemfahamu na akakukimbilia, hiyo ni dalili kwamba utapata kila kitu utakachokihitaji, biashara zako zitakuendea vizuri na mambo yako kukunyoonyekea.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Ukimsikia Njiwa analia kwa fujo Siku ya leo, basi hiyo ni dalili ya kupata habari mbaya au vituko vya kila mara kukutokea, unashauriwa kuwaona wazee kwa ushauri zaidi ili kujikiknga na mambo hayo.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Siku ya leo ukimuona au ukikutana na Mwanamme kabeba maji kwenye Ndoo, hiyo ni dalili ya kupata fedha kwa njia ya udanganyifu au utatapeli au utapata fedha kwa njia ya Rushwa au Magendo. Jihadhari na kukamatwa na usiwashirikishe ndugu zako.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Katika matembezi yako ya leo mchana ukimuona mtu anachota maji kwenye Kisima au Bomba au kwenye Mto au hata Baharini, hiyo ni dalili kwamba utapata fedha lakini hazitokaa kwa vile utazitumia katika mambo ya Anasa na Dhambi..

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Siku ya leo ukikutana na mtu anamwagilia maji katika shamba au bustani kwa kutumia Ndoo, hiyo ni dalili yakufunga ndoa na mwanamke tajiri na utanufaika na utajiri wake. Vilevile utapata habari ya mwanamke aliyejifungua mtoto wa kiume.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Siku ya leo ukimwona mtu anawanywisha Wanyama maji, basi ujue hiyo ni dalili kwamba kuna habari za uongo utaambiwa na Mkeo au Mpenzi wako kuhusiana na biashara zako. Jaribu kufanya uchunguzi kabla hujachukua hatua.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Siku ya leo ukikutana na mtu anamwaga Majivu, hiyo ni dalili kwamba mgonjwa wako aliye hospitali atapona au utaletewa habari ya nzuri za kupona ugonjwa wa mzazi wako wa kiume.

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Siku ya leo akikujia Yatima na akataka msaada wako, hiyo ni dalili ya kwamba mambo yako mengi yatakwama na kujikuta ukikosa msaada kutoka kwa watu uliowateemea.

0 comments:

Post a Comment