Mwanamuziki
Lady Jaydee jana amezuiliwa na Mahakama kuzungumzia jambo lolote lile
linalohusiana na Kampuni ya Clouds Media na Viongozi wa kampuni hiyo.
Amri
hiyo amepewa jana alipokwenda kusikiliza alichoitiwa Mahakamani hapo
baada ya viongozi wa Clouds media kwenda kufungua kesi dhidi yake.
Baada
ya kutoka katika Mahakamani alisema hiki
“Siruhusiwi
kuongelea zile ishu za wale watu niliotofautiana nao mpk mahakama
itakapotoa tamko. Hivyo sina jibu la swali lolote kwa sasa.”
Kwamujibu
wa Lady Jaydee anapaswa kurudi tena Mahakamani siku ya Jumatatu
Tarehe 27 mwezi May siku ambayo tamko litatolewa rasmi na Mahakama
juu ya Kesi iliyofunguliwa na viongozi hao wa Redio hiyo.
KUZIBWA
MDOMO
Kwa
upande wa Lady jaydee alikuwa amepanga kutoa taarifa zaidi juu ya
Viongozi hao wa Redio hiyo siku ya Tarehe 16/17 baada ya Kiongozi
mmoja wapo kuongea katika Redio yao juu ya bifu yao lakini zikiwa
zimesalia siku chache kutolewa kwa taarifa hiyo amri ya Mahakama
imemtaka kutozungumza chochote kile juu ya watu hao,kitendo hiki ni
sawa na kumziba mdomo mwanadada jaydee.
0 comments:
Post a Comment