Mwenyekiti
wa kampuni ya IPP Dr Reginald Mengi amesema kuwa kuanzia mwezi wa
tano huu atatoa pesa taslimu kiasi cha shilingi Milioni moja kila
mwezi kwa Tweet atakayochagua kuwa bora dhidi ya vita ya umasikini.
Mwenyekiti
amesema kuwa lengo lake kufanya hivyo nikutaka kupata mawazo
mbalimbali kutoka kwa watu ambayo atayatumia kupiga vita dhidi ya
Umasikini unaolitesa taifa la Tanzania na Afrika kiujumla.
“Umaskini
umekuwa sugu. Kwa mwaka1 anzia Mei ntatoa sh1m kila mwezi kwa tweet
nitakayochagua kuwa bora kushinda vita na umaskini”
Umasikini
ni jambo ambalo limekuwa kero kubwa sana kwa Mwenyekiti huyo kwani
siku ya Jumatano aliandika umasikini wa akili unadumaza uwezo wa
kuchambua mambo na kudaikuwa umaskini wa akili ni shamba walitumialo
wanasiasa.
“Umaskini
wa akili unadumaza uwezo wa kuchambua mambo...lipi uongo, lipi kweli.
Ndio sababu umaskini wa akili ni shamba la wanasiasa”
0 comments:
Post a Comment