Monday, May 27, 2013

KALA JEREMIAH APATA TUZO YA KWANZA


Mwanamuziki chimbuko la BSS Kala Jeremiah anaetamba katika miondoko ya Hip Hop hapa bongo kwa sasa na ngoma yake ya Dear God amepokea Tuzo ya kwanza ya Wimbo Bora wa Hip Hop katika Tuzo zilizoandaliwa na kampuni ya magazeti pendwa Tanzania.
Toka kala ameanza muziki hakuwahi kubahatika kupata tuzo yoyote ile lakini kwa mwaka huu kwake umeaanza vizuri kwa kupata tuzo hiyo wakati katika Kili Music Award ameteuliwa katika categories kadhaa hivyo ni mwazo mzuri kwake katika safari yake ya kuendelea kufanya poa katika tasnia ya muziki Bongo.
Toka nianze muziki jana ndiyo nimechukua tuzo yangu ya kwanza, tuzo hizi zimeandaliwa na global publishers.na ni tuzo ya wimbo bora wa hip hop.nasema asante mungu kwa shavu jingine, asante sana mashabiki kwa kura zenu, asante sana global publishers. na nawaomba mfanye hii kitu miaka yote ili kuwe na tuzo nyingi nyingi”
Hakuishia hapo Kala akatoa tena ombi jingine ambalo linakuja kwako na si mtu mwingine,likiwa na lengo la kumpigia kura tena na sii jambo lingine ili aweze kupata Tuzo nyingne kwa lengo la kupata heshima nyinginee,huyu hapa kala na si mtu mwingnee
ndugu zangu nawakumbusha kuendelea kunipigia kura kwenye tuzo za kilimanjaro music awards.asanteni sana kwa mara nyingine”

1 comments:

  1. umestahili Kala, hongera sana. Wimbo wako wa "Dear God" ni mzuri sana

    ReplyDelete