10:43 PM
Namba
hiyo iliyotajwa katika TAMKO imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba
hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012.
Hata
hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye
email zangu sehemu ya anuani.
Namba
hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke
yake.
Namba
hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.
Kama
JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata
taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.
Mambo 2,
ama
namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au
imewekwa
makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa
watu.
Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au
hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na
upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.
Napenda
kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza,
kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za
kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango
wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote
vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule.
Juhudi
zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo
haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.
Napenda
kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki
yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili
Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza
'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI
hutamalaki.
Mtu
yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka
kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda
mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.
Ni
muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki.
0 comments:
Post a Comment