Mfanyabiashara
maarufu jijini Arusha Joseph Sambeke mwenye umri wa miaka 49
alimaarufu kwa jina la Bob Sambeke amefariki dunia Juzi kwa ajari ya
Ndege ndogo aliyokuwa akiindesha.
Huu
ni msiba wa tatu kutokea jijini Arusha kwa wafanya biashara wa jiji
Hilo katika mwezi mmoja tu alianza kufariki Wakili na mfanyabiashara
maarufu Nyaga Mawalla akafuata mfanya biashara wa madini mkoni humo
Henry Nyiti na juzi umauti umemfika Sambeke.
Alijeruhiwa na baadaye alifariki akiwa njiani wakati akiwahishwa hospitalini na askari wa Magereza ambao wanaishi katika kambi alipoanguka. Mazishi yake yamepangwa kufanyika Alhamisi eneo la Karanga, Moshi.
0 comments:
Post a Comment