Tuesday, April 9, 2013

WABUNGE WAGOMA KUTOA POSHO YA SIKU MOJA TUU

Wabunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wamegoma kutoa posho yao ya siku moja tu kuichangia Timu yao ya Taifa,Taifa Stars kama motisha kwa timu baada ya Ushindi Dhidi ya Morrocco.

Akizungumza haya Mh Zitto Zuberi Mbunge wa Kigoma Alianza kwa kusema kuwa Taifa Stars Mtawaumbua tu.kauli hii inatoa picha wazi kuwa Mbunge huyo anatambua kuwa wabunge wenzake hawawezi kufanya jambo hilo
TaifaStars mtawaumbua tu! Hivi unaweza kuamini ukiambiwa Wabunge wamegoma kutoa posho yao ya siku moja kuchangia Timu ya Taifa kama motisha baada ya ushindi dhidi ya Morocco? Unaweza kuamini?”alihoji Zitto

lakini alikwenda mbali zaidi na kukumbusha Jirani zetu kenya jinsi wabunge wao walivyoonesha uzalendo na upendo kwa timu yao ha Harambee Stars walivyotoa sare na Nigeria jinsi walivyotuzwa na kuzawadiwa kama motisha kwa kazi nzito waliofanya,lakini timu yetu imeshinda wabunge wamegoma kutoa posho ya siku moja tuu kuwapa hamasa vijana wa Taifa stars.

Jikumbushe, Kenya #HarambeeStars wametoa sare tu na Nigeria, Zawadi walizopewa utadhani wameeenda CAN”






0 comments:

Post a Comment