Tuesday, April 9, 2013

PROFESOR JAY ATOA SABABU MUZIKI WA BONGO KUZOROTA

Msanii prof Jeezy,Heavy Weight Mc anaetamba katika Tasnia ya bongo Fleva toka Miaka ya Tisini mpaka sasa amefunguka na kusema sababu zinazofanya muziki wa bongo kuzorota na wasanii wengi wa bongo kupotea katika fani.

PROF ametupa lamawa zake kwanza kwenye vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na mchango mkubwa sanaa kumpa nafasi msanii lakini vyombo hivyo hivyo vya habari vimekuwa vikiua wasaniii na kazi za sana,kwani kuna watu katika vyombo hivyo wamekuwa na masirahi ya kwao binafsii,wanacheza nyimbo mbovu na wasanii wabovu huku wasanii wazuri na nyimbo nzuri zikikosa nafasi.

Vilevile hata mashabiki nao wanachangia kukuza muziki wetu hata kuuwa muziki kwani wao ndio huzipenda nyimbo hizo mbovu na kusurpot moja kwa moja aina ya muziki wanaoletewa na vyombo vya habari.

Sababu za Muziki wa Tanzania kuzorota kunachangiwa sana na Wasanii wenyewe, mashabiki kushabikia nyimbo mbovu, Media n Serikali”
vilevile aliendelea kusema kuwa Msalaba asibebeshwe mwanamuziki peke yake maana Media, Shabiki na Serikali nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa, Tukijirekebisha PAMOJA WE CAN

0 comments:

Post a Comment