Tuesday, April 9, 2013

KANYE WEST ASHTAKIWA

Msanii na Mtayarishaji wa muziki kutoka magharibi ya mbali Kanye West amejikuta katika wakati mgumu sanaa baada ya kushitakiwa kwa kutumia vionjo vya muziki alivyotumia katika ngoma yake ya “Gold Digger”bila kupata ruksa kwa wamiliki wa muziki huo.

Trena Steward na Lorenzo Pryor ni watoto wa David Pryor ambae ni mwandishi wa kazi hiyo original wamemshtaki Mahakamani Producer Kanye kwa kutumia baadhi ya vipande vya kazi hiyo bila kupata ruksa kutoka kwao.

Na kama watafanikiwa au kushinda kesi hiyo watoto hao watalipwa na Kanye kwa kuwa amekiuka utaratibu wa copyright,vilevile sheria haitaishia kwa Kanye pekee bali hata kwa wasanii wengine kama kikundi kinachoitwa Quest na Missy Elliot ambao nao pia wametumia vionjo hivyo katika kazi zao zilizofanyika . 
 
Source MTV BASE

0 comments:

Post a Comment