10:17 PM

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR
20)
Utapatwa na mambo ya ajabu ajabu, usijaribu kuvuka mto
usioujua kina chake kwani upo uwezekano wa kuondoka na maji. Tegemea
kupata safari ya ardhini itakayokupeleka sehemu ambayo hujawahi
kufika.
NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
LEO
biashara ni nzuri, ndoa itatimia ijapo yule anaehusika na mashauri
hayupo. kuna ishara nzur kazini au matembezini na upo uwezekano wa
kupata bahati huko uendako.
MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN
21)
Mambo yako yatatimia katika Jumatano, au mwezi wa nane . Ni
siku nzuri kwa kila jambo utakalolitenda. Unashauriwa kuanzisha mambo
mapya leo kwani ndiyo siku yako nzuri.
KAA – CANCER (JUN 22 –
JUL 23)
Unashauriwa kuwa uwe makini na marafiki wapya
watakaokujia siku za karibuni.Hakikisha unafanya sala kwa dini yako
au Fanya sherehe au pika chakula watu wale. Kufanya hivyo
kutakusaidia kuondokana na matatizo mbali mbali.
SIMBA – LEO
(JUL 24 – AUG 23)
LEO ni ya matatizo kwako usiogope taabu kwani
lazima taabu itakufikia kwanza ndio uone mafanikio baadae. jaribu
kuwa karibu na watu wa dini yako ili kubarikiwa na ikusaidie
kuondokana na matatizo yanayokukabili.
MASHUKE – VIRGO (AUG
24- SEPT 23)
LEO kuna dalili ya kuibiwa mali yako au kupoteza vitu
vya thamani kubwa, vilevile kuna ishara ya kukimbiwa na Mkeo au
Mpenzi wako au Watoto wako. Usiogope maadui hata kidogo.Kuna Mkuu
utakutana nae karibuni, shirikiane nae, atakusaidia sana na utapata
mafanikio,
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Kuna mambo
mabaya yanakujia katika biashara au kazi yako, Mipango yako yote
kuhusu biashara ifanya upesi itafuzu. Jihadhari na vikundi visivyofaa
hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili
wakusaidie.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Mambo yako
yamo hatarini kuharibiwa na wakubwa wa serikali au kidini, Itakubidi
ukutane na watu hao na kufanya mazungumzo nao, jaribu sana kupunguza
hasira na unatakiwa kuwa mpole kwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV - DES 21)
Unashauriwa
kutosafiria kwa muda huu ili kujikinga na mabalaa. Mgeni atakaporejea
ndio mambo yako mengi yatatengemaa. Jaribu kuwa muangalifu na yoyote
utakayeshirikiana naye.
MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN
20
Adui yako anayekusumbua lazima atapatwa na matatizo makubwa ya
Kiserikali au ugonjwa. unashauriwa kuutumia muda huu kukamilisha
mambo yako uliyokuwa umeyapanga kuyafanya.
NDOO –AQUARIUS
(JAN 21 – FEBR 19)
LEO utapata mkosi kazini kwako au utaletewa
biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha, Kuhusu safari uliyopanga
kwenda ina shida kidogo lakini usiogope.Pamoja na matatizo nenda hiyo
safari.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
LEO utapata
fedha au utapata faida ambayo hukuitegemea au utasamehewa madhambi
uliyomfanyia rafiki yako. Kuhama hama ni bora kuliko safari ndefu
unayotarajia kwenda.
0 comments:
Post a Comment