4:45 AM

Je
umejiuliza kwa nini hupati mafanikio kimaisha, mambo yako yanakwama
na unakosa unachokitaka. Unajaribu kila njia kupata mafanikio lakini
inashindikana?
Mojawapo ya mambo yanayokuangusha kimaisha ni
Tabia yako, ukifikiria unaweza kufanya jambo utafanya, na ukifikiria
kwamba huwezi kufanya hutoweza, je ni kwa nini?
Jibu hilo
linapatikana katika nyota na maelezo yake ni kama ifuatavyo:
WATU
WA NAMBA 1:
Ukiwa umezaliwa tarehe 1, 10, 19 au tarehe 28 au
jina lako likianzia na A J S, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio
kwanza kabisa linatokana na tabia ya Unyonge na kutegemea sana watu
achana nayo.
Pili acha kujivuna, acha kuringa na usipende
kuwa kimbele mbele katika mazungumzo, Tabia hiyo inawafanya watu
wakukimbie.
Tatu tabia yako ya kutokuwa na subira,
kulazimnisha mambo na kujisifu haikusaidii achana nayo kabisa.
WATU
WA NAMBA 2:
Ukiwa umezaliwa tarehe 2, 11, 20 au tarehe 29 au
jina lako likianzia na B K na T, tatizo lako kubwa la kukosa
mafanikio kwanza kabisa linatokana na wewe kuwa na aibu sana na kuto
kujiamini.
Pili unatakiwa utumie nguvu wakati mwingine katika
mambo yako bila hivyo huwezi kupata.
Tatu tabia yako ya
kupenda kujishughulisha na mambo madogo madogo, kutoa mawazo ambayo
hayaendani na hali halisi, na tabia yako ya kutokueleweka na kupenda
kusema uongo haikusaidii , achana nayo.
WATU WA NAMBA
3:
Ukiwa umezaliwa tarehe 3, 12, 21 au tarehe 30 au jina lako
likianzia na C L na U, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza
kabisa linatokana kuwa na matamanio makubwa kupita kiasi au kutokuwa
na matamanio kabisa.
Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya
kujionyesha mbele za watu kwamba wewe unajua zaidi kuliko wao.
Tatu
tabia yako ya kutaka kudhibiti watu katika mambo yako au katika dili
zako inawafanya watu wakukimbie.
WATU WA NAMBA 4:
Ukiwa
umezaliwa tarehe 4, 13, 22 au tarehe 31 au jina lako likianzia na D M
na V, tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana
na wewe kuto jishirikisha na Jamii na kutokuelewa mabo kwa
haraka.
Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kushindwa
kuonyesha hisia zako
Tatu, achana na tabia yako ya kufanya
mambo yasioeleweka hasa kuwa mkali au kununia watu.
WATU WA
NAMBA 5:
Ukiwa umezaliwa tarehe 5, 14, au tarehe 23 au jina
lako likianzia na E, N na W tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio
kwanza kabisa linatokana malengo, dhamira au mwelekeo tangu mwanzo wa
maisha yako
Pili unatakiwa uachane na tabia yako ya kuwa na
jambo au mtu kwa muda mfupi. Kaa na watu acha kubadili marafiki kila
leo
Tatu, tabia yako ya ulevi, ngono, kucheza kamari, kutokuwa
muangalifu, ukosefu wa adabu na tabia ya kuchelewesha mambo
inachangia wewe kukosa mafanikio.
WATU WA NAMBA 6:
Ukiwa
umezaliwa tarehe 6, 15 au tarehe 24 au jina lako likianzia na F O na
X tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana
Usumbufu, Ubinafsi na Wivu
Pili unatakiwa uachane na tabia
yako ya kusengenya watu na kuingilia mambo ya watu wengine bila hivyo
huwezi kufanikiwa.
WATU WA NAMBA 7:
Ukiwa umezaliwa
tarehe 7, 16, au tarehe 25 jina lako likianzia na G P na Y tatizo
lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana kuwa na tabia
ya kuwafikiria wenzio mabaya na kutomwamini mtu yoyote
Pili
unatakiwa uachane na tabia yako ya kutumia ujanja ujanja katika
mambo, uongo au njia za kitapeli kupata fedha.
Tatu tabia yako
ya ulevi, Dhihaka, Kupiga vijembe vinakusababisha kukosa
mafanikio.
WATU WA NAMBA 8:
Ukiwa umezaliwa tarehe 8,
17, au tarehe 26 au, jina lako likianzia na H Q na Z tatizo lako
kubwa la kukosa mafanikio kwanza kabisa linatokana kutokuelewana na
watu na kujifanya kuwa na hisia za huzuni wakati wote, uroho na
ulafi, zinakusababisha kukwama.
Pili unatakiwa uachane na
tabia yako ya kupenda kujilimbikizia mali, ubahili Uliokithiri na
kupenda kuchokoza watu au kuudhi watu vitakukwamisha.
WATU WA
NAMBA 9:
Ukiwa umezaliwa tarehe 9, 18, au tarehe 27, jina lako
likianzia na I na R tatizo lako kubwa la kukosa mafanikio kwanza
kabisa linatokana na wewe kushindwa kudhibiti maamuzi ya ghafla,
hasira za haraka haraka, na unywaji wa pombe
Pili unatakiwa
uachane na tabia yako ya kuongozwa na watu wengine na kupenda
kubembeleza
Tatu tabia yako ya kupenda ugomvi na ndoto ambazo
hazina malengo kunasababisha wewe kukwama kabisa kimaisha.
0 comments:
Post a Comment