9:58 PM
PUNDA- ARIES (MACH 21- APR
20)
Leo inaonekana una furaha na hupendi mtu yoyote akukasirishe,
lakini jiepushe sana na marafiki au washirika ambao unaona
watakukasirisha. Inaonekana hao marafiki wanadhamira ya kukuudhi.
Tafuta sababu yoyote ya kuwakwepa.
NG’OMBE –TAURUS (APR 21
– MAY 20)
Umefanikiwa kujiepusha na kufanya maamuzi mazito sana
katika kipindi cha mwezi mzima uliopita. Inaonekana kabisa kwamba
ndani ya moyo wako unajua kabisa kitu gani cha kufanya na ukifanye
lini lakini unashindwa kufanya kwa sababu unataka kumhifadhi mtu./
Mwezi huu amua moja.
MAPACHA – GEMIN (MAY 21 – JUN 21
Kuna jambo la kukufurahisha limekutokea kazini na limekufanya
uache mambo yote ili kulishughulikia. Kama utajisikia umechoka
kiakili fanya mazoezi au kimbia au tembea tembea. Kuna uwekezakano wa
kukutana na rafiki au mshirika wako ambaye atakufanya ufurahie maisha
wiki hii.
KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 22
Leo inaonekana
kuwa alkhamisi itakayokuwa na matatizo kwako, jitahidi kufanya
machache utakayoweza ili kuepukana na matatizo. Jiahidi wewe mwenyewe
kwamba utatekeleza majukumu yaliyobaki wiki ijayo. Uwezekano wa
kutekeleza upo unachotakiwa kufanya ni kutumia akili na
ujasiri.
SIMBA – LEO (JUL 23 – AUG 22)
Inaonekana ni
siku ya mapenzi na mahaba kwa sababu sayari ya mwezi inaingia katika
nyota yako.Hii vile vile inaonyesha kwamba mazingira yatakuwa tofauti
na unavyofikiria hivyo kuwa muangalifu sana na watu
usiowafahamu.
MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama
mpenzi wako anakulalamikia kwamba hakupati vile inavyotakiwa
kubaliana nao kwa sababu wanasema ukweli.Sayari ya Zohal imesimama
katika nyota yako na ndio inakufanya usiwe na muda kushughulikia
masuala ya mapenzi. Wafanye uwapendao wajue jinsi unavyoshughulika,
hiyo ndio njia ya kuwa nao karibu.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24-
OCT 23)
Leo unaonekana una mambo mengi yanayokushughulisha kama
ilivyokuwa wiki iliyopita na shughuli za kazi zimeongezeka kidogo.
Fikiria sana Je hizi kazi kuna mtu anakujazia uzifanye au unazifanya
kwa ajili ya kuinua hadhi yako? Kama ni la kwanza tafuta sababu ya
kukwepa kama ni la pili jipunguzie majukumu utaumia.
NGE -
SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Hii ni siku nzuri kama ukiwa na mpango
wa kununua Nyumba au gari au kitu chochote. Manunuzi yote makubwa
yana baraka zote ukiwa wewe mwenyewe au ukiwa na mshirika wako. Kama
unafanya kazi Benki au katika kampuni ya Bima huo ndio wakati hasa wa
kufanya mipango yako ya kimaisha.
MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23
- DES 21)
Wiki hii fanya mawasiliano na jamaa zako walio nje ya
nchi. Kama kazi zako zikiwa zinahusiana na wageni utapata nafasi
nzuri itakayokushangaza. Kama una mpenzi anaishi nje, basi tegemea
kupata habari za kufurahisha za mualiko wa kumtembelea.
MBUZI
- CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Leo Sayari ya jua inaingia katika
nyota yako na hiyo inashiria kuanza kufunguka kwa mambo yako
yaliyokwama, utapata marafiki wengi wa jinsia tofauti na yako ambao
watakuburudisha na kukufurahisha. Ni wakati mzuri wa kufanya
starehe.
NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Je
unatafuta mpenzi? Sayari zote zinazohusiana na mambo ya mapenzi ziko
kwenye nyota yako wiki hii. Utapata wapenzi wapya, waliotoroka
watarudi, waliowakorofi wataacha ukorofi wao na waliokukatalia
watakubali. Tumia wakati huu kujifurahisha.
SAMAKI – PISCES
(FEB 20- MACH 20)
Ni siku nzuri nzuri na ya bahati kwako
ukishindwa kutumia bahati hiyo usijilaumu, wala usiseme umetengwa.
Toka tafuta nafasi, fanya uhusiano, waendee wenye pesa wakukopeshe,
fanya biashara, anza kujenga, nunua nyumba na chochote. Changamka
usilale
0 comments:
Post a Comment