![]() |
Mwenyekiti wa kamati ua ujenzi wa eneo la mtaa wa mafia Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiongea na waandishi wa habari, kulia ni Katibu Mku wa Yanga Lawrence Mwalusako |
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la Yanga SC, liliopo Mtaa wa
Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam, Ridhiwani Jakaya Kikwete ameteua
Wajumbe kadhaa wa kumsaidia kazi hiyo, wakiwemo wanasheria wawili na
wataalamu wa Taasisi za Fedha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya
Twiga na Jangwani, Ridhiwani alisema katika uteuzi wa Kamati hiyo,
amezingatia utaalamu, uzoefu na mahusiano mazuri na watu.
Ridhiwani
mesema kwamba kutakuwa na Kamati mbili za kushughulikia mchakato huo,
moja ikiwa ya wataalamu na nyingine ya watendaji.
Aliwataja
Wajumbe wa Kamati ya Wataalamu kuwa ni Makamu wake, Issa Hajji Ussi
na Wajumbe Isaac Chanji, Mbaraka Igangula, Jaji John Mkwawa, mtumishi
ya Beki ya Uwekezaji Tanzania (T.I.B.), Alan Magoma,
Mwanasheria mkongwe, Mavale Msemo na mtumishi mwingine wa Benki,
Charles Palapala.
“Utaona
kuna watu wengi wa taasisi za fedha, kwa sababu hili zoezi linahitaji
fedha, tutaangalia kama tutaingia ubia na mtu, au sisi kama klabu
tukawekeza kwenye mradi huo moja kwa moja,”alisema.
Kwa
upande wa watendaji, Kikwete alisema kwamba Kamati yao itaongozwa na
Katibu wa Yanga SC, Lawrence Mwalusako, Beda Tindwa na Mahmoud
Milandu.
“Kamati
yetu sisi itakuwa ya kukaa na kutengeneza mipango na baadaye kama
kutakuwa na barua ya kupeleka wapi, au mtu wa kufuatwa, basi ile
kamati nyingine ndogo, itafanya kazi hiyo,”alisema.
{Source Yanga Website}
0 comments:
Post a Comment