Monday, April 15, 2013

LAKI SI PESA WAPIGWA MARUFUKU


Lilekundi maarufu sana hapa Town la wadada wanaocheza muziki huku wakiwa wamevaa kanga moja alimaarufu kama Kanga moja Laki si Pesa waliokuwa wakifanya kazi yao hiyo katika kumbi mbalimbali za starehe na kujaza watu ambao ni wapenzi wa maonesho hayo limepigwa marufuku kuendelea kufanya matamasha hayo jana.

Serikali imepiga marufuku kundi hilo kutokana na ukweli kwamba linauwa utamduni wa kitanzania na kuchochea vitendo vya anasa kwani aina ya uchezaji si sahihi na vinahusishwa na ukahaba tu.

Laki si pesa ni kundi lililokuwa likipingwa na watu mbalimbali kutokana na namna wadada hao walivyokuwa wakicheza,walihusishwa na vitendo vya kuchochea vitendo vya Ngono,kuhamasisha vitendo hivyo kwa wale wanaokuwa wakiangalia show za Laki si pesa lakini hata wabunge kwa mara ya kwanza wabunge walionesha kukerwa na kundi hilo na kudai kuwa wanachangia kuporomosha maadili ya Kitanzania.

Kundi la Laki si pesa limepigwa marufuku jana katika bunge la jamhuri ya muungano.


0 comments:

Post a Comment