10:08 PM
PUNDA- ARIES (MACH 23- APR
20)
Siku ya leo utapatwa na mambo ya ajabu ajabu, mambo hayo
yatakushangaza usijaribu kujibishana na watu usiowajua kunaweza
kutokea ugomvi mkubwa.Wiki hii utapata safari ya ardhini
itakayokupeleka sehemu ambayo hujawahi kufika.
NG’OMBE –
TAURUS (APR23 – MAY 20)
Leo upo uwezekano wa kukutwa na balaa
huko uendako.kuna uwezekano wa kutokea matatizo kazini kwako au kwa
mtu anayekuhusu. hasa ukikutana na Mbeba mizigo,
MAPACHA -
GEMINI (MAY 23- JUN 23)
Leo hii au wakati wowote ukikutana na
Mhubiri, basi itakuwa ni siku nzuri kwa kila jambo utakalolitenda.
Unashauriwa kuanzisha mambo mapya leo kwani ndiyo siku yako
nzuri.
KAA – CANCER (JUN 22 – JUL 23)
Wiki hii
uhusiano wako na mtu uliyempata hivi karibuni awe ni mpenzi au rafiki
utavurugika, Unashauriwa kuwa makini na hao marafiki wapya
watakaokujia siku za karibuni.
SIMBA – LEO (JUL 24 – AUG
23)
Wiki hii ikitokea ndugu yako au mpenzi wako aliyekukosea
akikuomba radhi au akataka umsamehe, basi hiyo ni dalili kuwa watu
wengi wanakukubali kwa kazi zako nzuri unazozifanya, jaribu kuwa
karibu na watu wa dini ili kubalikiwa mambo yako.
MASHUKE –
VIRGO (AUG 24- SEPT 23)
Leo hii ukikutana na mtu ambaye hana miguu
kabisa, hiyo ni dalili kuibiwa mali yako au kupoteza vitu vya thamani
kubwa, vilevile ni ishara ya kukimbiwa na Mkeo au Mpenzi wako au
Watoto wako.
MIZANI - LIBRA (SEPT 24 – OCT 23)
Ukikutana
na mtu mwenye makovu ya moto Leo hii, hiyo ni dalili kuwa kuna mambo
mabaya yanakujia katika biashara au kazi yako, jihadhari na vikundi
visivyofaa hasa nyakati za jioni. Jaribu kuwasiliana na wataalamu ili
wakusaidie.
NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Leo hii
ukikutana mtu mguu wa bandia , hiyo ni ishara kwamba mambo yako yamo
hatarini kuharibiwa na watu wakuwa wa serikali au kidini, unatakiwa
kuwa mpole kwa muda huu ili kupisha dhahama hiyo.
MSHALE -
SAGITARIUS ( NOV - DES 23)
Siku ya leo na wiki hii unashauriwa
kutosafiria ili kujikinga na mabalaa katika safari hizo. Jaribu kuwa
muangalifu na yoyote utakayeshirikiana naye. Leo hii ukikutana na Mtu
anayechechemea, hiyo ni ishara ya kupata matatizo,
MBUZI -
CAPRICORN (DES 22 – JAN 20
Leo hii katika matembezi yako
ukikutana na mtu kajipamba Maua, hiyo ni dalili ya kufanikiwa katika
mambo yako, unashauriwa kuutumia muda huu kukamilisha mambo yako
uliyokuwa umeyapanga kuyafanya.
NDOO –AQUARIUS (JAN 23 –
FEBR 39)
Leo ni siku mbaya kwako kuna uwezekano wa kupata mkosi
kazini kwako au utaletewa biashara ambayo itakuletea balaa kimaisha.
Jaribu kuwa muangalifu mipango yako yote uliyoipanga wiki hii achana
nayo.
SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo hii katika
biashara zakoutapata faida ambayo hukuitegemea na yule rafiki yako
uliyemkosea utakusamehe madhambi uliyomfanyia. Jitahidi kukutana na
wakubwa zako wakusaidie kupata ushauri.
0 comments:
Post a Comment