Thursday, April 11, 2013

NYOTA YAKO LEO ALKHAMISI 11/4/2013

PUNDA- ARIES (MACH 21- APR 20)
Mawazo yako hivi sasa ni kusafiri na unafanya kila njia kushirikisha watu ili safari hiyo ifanikiwe. Safari ipo na itakuwa. Leo jioni hutopata uzito wa kumpata mtu wa kuwa nae katika kipindi hicho. Utatfutwa kusuluhisha ugomvi wa rafiki yako kuwa tayari kumtetea.


NG’OMBE – TAURUS (APR21 – MAY 20)
Mipango yako kabambe uliyoipanga inaweza ikageuka ikawa balaa au vurugu na unatakiwa usiwe mgumu katika kubadili mipango hiyo inapobidi.Kama itakuwa unasisitiza kutobadilika basi itakuwa ni kuvurugika kwa mambo yako yote.

MAPACHA - GEMINI (MAY 21- JUN 21)
Utapata nafasi ya kukutana na viongozi wako, itumie vizuri nafasi hiyo kuweka sawa mambo yako ya kimaisha. Elewa kwamba sayari ya Jupiter itakuwa katika nyota yako kwa muda wa miezi kadhaa na hiyo inaashiria kupata safari za ghafla za hapa na pale. Jitahidi kutumia nafasi hiyo kujinufaisha.
.
KAA - CANCER (JUN 22- JUL 22)
Leo itakuwa siku nzito kwako, inamaanisha hata mambo yako na matamanio yako yatakuwa mazito kwa hiyo usijaribu kufanya lolote, Jaribu kutumia wakati huu kuwa na familia yako kwa matembezi hasa wakati wa jioni.

SIMBA - LEO (JUL 23 –AUG 22)
Utapata furaha ya kurudishwa kazini au katika biashara au mpenzi wako kurudi. Kama uko kazini jaribu kumalizia kazi zinazokukabili na usijaribu kukwaruzana na wafanyakazi wenzio. Elewa kwamba hao unaofanya nao kazi wamekuchoka kama wewe ulivyowachoka.

MASHUKE - VIRGO (AUG 23- SEPT 23)
Kama kaka yako au dada yako anataka kuzungumza habari nyeti na wewe tafadhali kwa njia yoyote ile msikilize, lakini jaribu kuficha mawazo yako. Jambo lolote ambalo utaliamua leo unaweza kulibadili hapo baadae. Jitayarishe kwa majaribu.

MIZANI - LIBRA (SEPT 24- OCT 23)
Weka masikio yako wazi, kuna mtu utapata habari zake na anaweza kukusaidia kupata fedha. Wakati huu Sayari za Mwezi na Uranus zinatembelea nyota yako na ndio wakati wako wa kupata fedha. Fanya mipango ya Fedha sasa na zungumza na watu wenye fedha utapewa Mkopo.

NGE - SCORPIO (OCT 24- NOV 22)
Jaribu kutekeleza majukumu yako yote leo kabla jua halijazama. Nyota haziwezi kukupa nafasi katika kipindi kinachokuja. Utaona kwamba mipango mingi itakwama na watu hawatokupa msaada unaohitaji. Ni vyema ukawa kivyako katika muda wa wiki moja mpaka balaa hilo liondoke.

MSHALE - SAGITARIUS ( NOV 23 - DES 21)
Jaribu kuwa mtulivu kama mpenzi wako au mshirika wako au mmoja wa watu ndani ya famila yako akidhamiria kukuacha.Ni kweli watakuwa na sababu nzito za kufanya hayo lakini njia watakazozichukua haziridhishi. Hivi sasa utahitaji sana kutumia busara ili kuepusha migongano.

MBUZI - CAPRICORN (DES 22 – JAN 20)
Hali ya wasiwasi inayokukabili bado ipo. Inaonekana kuwa wewe ni mtu unayependa sana amani na unataka sana kufanya Amani. Pamoja na kwamba utahisi kwamba juhudi zako hazithaminiwi utapata faraja mwisho wa siku baada ya mchango wako kuthaminiwa.

NDOO –AQUARIUS (JAN 21 – FEBR 19)
Sayari ya Venus inaingia kwenye nyota yako wiki ijayo na hiyo ni dalili ya kunyooka kwa mambo yako ya kimapenzi. Kipindi hiki itakuia urahisi sana kupata mpenzi mpya au kutengeneza tena uhusiano ambao umevunjika kati yako na mkeo au mpenzi wako.

SAMAKI – PISCES (FEB 20- MACH 20)
Leo utapata majukumu mengi ya nyumbani. Jaribu kutumia uwezo wako wa ushawishi kuwafanya wengine waone dhamira yako. Fanya kazi zako kutoka nyumbani. Tafuta mipango mipya na biashara mpya ili uweze kuvutia wateja wa aina nyingine.


Imeandaliwa na Mtabiri Maalim Hassan


0 comments:

Post a Comment