Ile
filamu ya Love & Power ambayo imekuwa ikisubiriwa kwa hamu na
wapenzi wengi wa filamu hatimaye mwisho wa wiki hii siku ya Ijumaa
tarehe 12th
April 2013 itazinduliwa na kuingia sokoni rasmi na kusambazwa nchi
nzima na kampuni ya mahiri ya usambazaji wa filamu ya Steps
Entertainment Ltd.
Akizingumza
na waandishi wa wanahabari mratibu wa filamu ya Love & Power
Bwana Myovela Mfwaisa amesema kuwa “Filamu ya Love &
Power ni filamu ya mwisho kutengenezwa na marehemu The
Great Kanumba
inaingia sokoni na kuwafikia watanzania wote siku ya ijumaa,”
Hivyo
basi hii itakuwa fursa pekee kwa wa tasnia ya filamu na watanzania
wote kwa ujumla na kuweza kujionea kazi bora iliyotengenezwa na gwiji
la filamu na balozi aliyetangaza tasnia ya filamu ya Tanzania nje ya
mipaka ya Tanzania, kila mpenzi wa filamu aweke ahadi kutokuikosa
filamu bora na ya mwisho kuigizwa na marehemu nyota wa filamu
Tanzania.
Akizungumzia
kwa ufupi juu ya filamu ya Love & Power Bwana Myovela, “Filamu
ya Love & Power imetengenezwa na kampuni ya Kanumba the Great
film kwa kushirikia na Steps Entertainment Ltd ikiwa imeandikwa na
Ally Yakuti, Filamu ya Love & Power imeshirikisha wasanii nyota
katika tasnia ya Filamu Tanzania kama Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’,
Irene Paul, Patcho Mwamba, Grace Mapunda, Hartman, Rammy Galis pamoja
Seth Bosco ambaye ni mdogo wake na marehemu kuongozwa na Steven
Kanumba, Watayarishaji wakuu ni Steps Entertainment Ltd imetengenezwa
hapa jijini Dar es Salaam katika maeneo tofauti tofauti.
Lugha
iliyotumika katika filamu hiyo ni Kiswahili lakini pia Lugha ya
kiingereza imetumika kama ‘Subtitles’.
Umri wa kutazama filamu ya Love & Power ni miaka 16 ni filamu
nzuri inayotazamwa na watoto pamoja na familia, iliyopewa kibali cha
ukaguzi Kutoka Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza
Tanzania.
Katika
kuhakikisha kuwa wasanii wanafaidika na kazi zao tunaomba kila mdau
wa filamu awe mlinzi wa kazi hizi za filamu za kitanzania kwa
kupambana na Maharamia wa Power kwa kuwasiliana na Wasambazaji kwa
namba hizi: 0716 788 805, 0713 570 581kazi za Wasanii wa
filamu, pia tunawaomba wapenzi wa filamu kununua nakala halali yenye
nembo ya Steps Entertainment Ltd, hiyo itachochea maslahi kwa wasanii
wa Tanzania na kuongeza ajira kwa vijana ili kufikia hilo nunua
filamu ya Love & Power halali.
0 comments:
Post a Comment