Thursday, April 11, 2013

MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI CAG AMEWAKILISHA REPORT LEO

mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali CAG leo amewakilisha Report bungeni Jijini Dodoma na haya ni baadhi ya mambo yalikuwepo katika Report hiyo.

Kwa mujibu wa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kupita report yake iliyowasilishwa leo bungeni amesema kuwa misamaha ya kodi imeongezeka Kwa asilimia 78% kutoka mwaka 2011 mpaka 2012 kwa mwaka 2012 misamaha ya kodi ilikuwa Tshs 1.8 Tirioni Sawa na asilimia 27% ya makusanyo yote wakati Mwaka 2011 misamaha ilikuwa Tilioni 1,sawa na asilimia 18%.

CAG amesema kuwa suala la ucheleweshaji wa Fedha za miradi ya maendeleo zimepelekea Tshs 299 bilioni na $213milioni kutotumika Kabisa katika mwaka wa 2012.

Malipo tata ya TBC Kwa niaba ya StarMedia Tshs 618 Millioni vilevile maelfu ya vitabu yamekwama Bandarini Kwa kukosa ushuru toka mwaka 2009 hivi ni vitabu vya watoto vilivyopaswa kutumika ....

Wafanyakazi wa serikali za Mitaa wanakopa mpaka wanabaki hawana kipato Kabisa. Wafanyakazi 17,710 wamekutwa hawana salaries kwani wamekopa mpaka hawapati mishahara yao.

Hata hivyo Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG amesema kuwa serikali imepata hasara ya Tshs 578bn Kwa kudhamini Madeni holela

0 comments:

Post a Comment