Meneja
na Mtayarishaji wa Filamu katika nchi mbalimbali za Africa Prince
Richard Nwaobi aliekuwa akisimamia kazi za Marehemu Steven Kanumba
amewataka wasanii wengine wa Filamu Tanzania kuondokana na Fikra
potofu kuwa Lugha ya Kiiingereza ni tatizo katika soko la Filamu
kimataifa.
Meneja
huyo aliyasema hayo siku ya maazimisho ya mwaka mmoja toka kufariki
kwa Msanii Kanumba,aliwapa mfano wasanii hao kuwa hata Kanumba
aliweza kufanikiwa kufanya vizuri kimataifa kwa lugha yake nzuri ya
kiwsahili na sii kiengereza kama ambavyo dhana hiyo imewaka wasanii
wengi na kuwafanya kuwa waoga kujalibu kufunga katika soko la
kimataifa.
Aliendelea
kusema kuwa amejitaidi sana kudhuru Tanzania kwa lengo la kutengeneza
umoja kati ya wasanii wa Tanzania na Nchi zingine ili kuweza kuteka
soko la kimataifa lakini mwamko kwa wasanii kutoka Tanzania umekuwa
ni mdogo mnoo ukilinganisha na jitihada alizokuwa nazo Marehemu
Kanumba katika Kufikia malengo ya kufanya kazi Kimataifa.
“Wasanii
wa Tanzania hawawezi kufuata nyayo za marehemu Kanumba kwa sababu
wanahofu ya kutojua Lugha ya Kiingereza hawatambui kuna wasanii
maarufu wengi ulimwenguni hawajui Kiingereza kabsaaa lakini wanafanya
kazi ya sanaa na kufanikiwa duniani pasipo kutumia lugha ya
kiingereza.
Mbali
na suala la Lugha lakini pia aliwahasa wasanii wa Filamu nchini kuwa
wanapaswa kuwa na uongozi mzuri utakao simamia kazi zao za sanaa na
wao kuendelea kujifua kwa kazi zaidi hii itawafanya kufanikiwa zaidi
katika kazi yao ya sanaaa.katika
kumbukumbu za mwaka mmoja za kifo cha The Great Kanumba Meneja wake
huyo aliongozana na wasanii wengine kutoka nchini mbalimbali ili
kuazimisha kumbukumbu hizo na kuonesha upendo waliokuwa nao kwa
Kanumba the great.
![]() | |
| Prince Richard Nwaobi akiwa na Seth Bosco mdogo wa marehemu kanumba. |







0 comments:
Post a Comment