Miss
Tanzania aliewahi kushinda Miss World Africa mwaka 2005 Nancy Sumari
ameeleza sababu zilizomsukuma kuandika Kitabu Cha Nyota yako
alichokiandika kwa lengo la kuwafunza Wanafunzi kujifunza katika watu
waliowazunguka katika maisha yao ya kila siku.
Nancy
amesema kuwa alipopata mtoto wake wa kwanza ndipo alipata msukumo wa
kuona anafanya jambo litakalo wajengea watoto uwezo wa kujifunza
kutoka kwa watu wanaowazunguka katika maisha ya kila siku.
Mbali
na malengo ya kutunga kitabu ambayo kwa asilimia kubwa ameyafikia
lakini lengo kwa sasa ni kuona watu,watoto pamoja na wanafunzi
wanakuwa na utamaduni wa kujisomea Vitabu,hivyo atakuwa akifanya
Usomaji shirikishi kwa kuzunguka shule tofauti tofauti na kusoma na
wanafunzi pamoja lengo kuu ni kujenga utamaduni wa kujisomea kwa
wanafunzi ili wajifunze mengi zaidi.
Nacy
aliendelea kusema kuwa katika watu waliofanikisha yeye kufikia lengo
la kuandika Kitabu hicho ni Mwandishi Shabani Robert kwani anapenda
sana uandishi wake na kupenda kazi zake zilizo mpa mwanga yeye
kufikia Malengo hayo.







0 comments:
Post a Comment