Msanii
maarufu kutoka Tanzania alietamba sana na Style ya TAKEU nchini
Afrika Mashariki na kuweza kufanikiwa kufanya Shows Kibao ndani na
nje ya Tanzania Mr Nice hivi sasa amepata Shavu katika nchin ya Kenya
kwa kufanya kazi chini ya kampuni ya GROUND PA FAMILY chini ya
Msimamizi REFIGA.
Kwa
mujibu wa Meneja wa MR NICE MR REFIGA ambae anameneji wasanii kama
DNA,MR NICE na wasanii wengine kutoka Kenya amethibitisha kufanya
kazi na Msanii Mr Nice toka Tanzania na kusema kuwa wao wanafanya
kazi hivyo ikitokea kuna mtu atakuwa teyari kufanya kazi na Mr Nice
kutokea GROUND PA FAMILY mILANGO ipo wazi.
Mpita
Njia alifunguka na kumcheki msanii DNA tokea kenya ambae kwa sasa
anafanya kazi pamoja na Mr Nice chini ya Kampuni moja ya Ground Pa
Family nae alisema kuwa ni kweli kampuni yao imeamua kufanya kazi na
Mr Nice japo hakutaka kufunguka mambo mengi na kutupa mwongozo wa
kumcheki Boss wao ambae ni REFIGA.
Lakini
kwa kumbukumbu yangu kabla ya Mr nice Kuibukia Nchini Kenya CHINI ya
Usimamizi Mpya Makini wa kazi yake alikuwa na makubaliano ya kufanya
kazi na Producer Lamour Kutokea Fishcrub na makubaliano yalikuwa ni
kufanya ALBUM nzima baada ya muda mfupi baada ya makubaliano hayo Mr
NiCE ALIACHIA Tracks kadhaa ambazo azikuweza kupenya vizuri katika
soko la muziki wa Kitanzania na kuweza kumrudisha katika PICK YAKE.
Matumani
yangu ni kuwa Ground PA Family wameona kuwa Mr Nice anauwezo wa juu
katika kufanya muziki ndio maana wameamua kumpa dili hilo ya kusaini
Mkatba Chini ya GROUND PA FAMILY hivyo tusubili mambo mazuri ya Nice
akiwa katika uongozi mpya na menejimenti Mpya .
0 comments:
Post a Comment