Wednesday, April 24, 2013

RAISI JOYCE BANDA ATETA JAMBO NA MUGABE

JOYCE BANDA AKIWA NA ROBERT MUGABE
Raisi wa Nchi ya Malawi Joyce Banda jana usiku alikutana na Raisi wa Jamhuri ya Zimbambwe Mh Robert Mugabe na Kunena juu ya kuweka Mahusiano mazuri kati ya Malawi na Zimbambwe na kuweka nia ya kutaka kukuza Uchumi wa NCHI hizo mbili.
 
sote tulikuwa tukiangalia mahitaji ya nchi zote mbili kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kama nchi zenye ubia kibiashara kwani nchi zote mbili zimepitia matatizo ya kiuchumia,hivyo itakuwa vizuri kama tutashirikiana na kubadilishana ujuzi na uelewa ili kuboresha maisha ya Raia katika nchi zote mbili”

aliendelea kusema kuwa anaona ameheshimiwa kukaribishwa katika ufunguzi wa 54 wa Biashara za Kimataifa wa Zimbambwe utakaofanyika siku ya Ijumaa.

Mimi wa Raisi Dr Joyce Banda nalichukulia suala hili kama nafasi nyingine kwa Nchi ya Malawi kuonesha Bidhaa zake kama sehemu ya kutangaza Biashara katika Nchi yetu.Alisema Joyce Banda Raisi wa Jamhuri ya Malawi




0 comments:

Post a Comment